ntukula michuzi

Saturday, January 11, 2014

MTOTO WA AJABU DAR

MTOTO WA AJABU DAR

Na Hamida Hassan na Imelda Mtema
AMA kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao, Andrea Marcus (13), mkazi wa Mbezi-Kibanda cha Mkaa, Dar anadaiwa kuwa wa ajabu kutokana na vitendo vyake.
Mtoto huyu amedaiwa kuwa ni wa kichawi kutokana na maajabu yafuatayo:
Mkazi wa Mbezi-Kibanda,  Andrea Marcus.
Ana uwezo wa kula ubwabwa sufuria moja la familia, anamudu kunywa maji ndoo moja, ana uwezo wa kuingiza tumboni mikate mikubwa saba kwa mlo mmoja,  amewahi kula mchele (si ubwabwa) ndoo nzima.
Mbaya zaidi baada ya kula milo hiyo huwa haoneshi ameshiba.
Maajabu mengine ambayo yanawashangaza watu wanaoishi naye ni jinsi anavyokula chakula kwa kumwaga chini kisha kukomba mpaka udongo.
“Sina amani ya moyo, naomba Watanzania wanisaidie, mwanangu ananiuma sana, hata kujisaidia ni hapohapo, chakula anakula kupita kiasi, kama nilivyosema hashibi na bado hali kama mwanadamu wa kawaida,” alisema mama wa mtoto huyo.
Akizungumzia madai ya uchawi, mama huyo, Angelina Marcus alisema mwaka 2001 alimzaa Andrea katika mimba ya miezi nane kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar.
“Nilipofika nyumbani tu, alikuja mwanamke mmoja, akasema amekuja kunipa hongera. Wakati anaingia alianguka, kichwa ndani miguu nje, alipoamka akaaga akisema anakwenda kuniletea kisamvu.
“Mama yangu akamwambia mzazi hali kisamvu, kama anataka akanichinjie bata. Yule mwanamke aliondoka, hakurudi tena,” alisema mama Andrea.
Aliendelea kudai kuwa, baada ya wiki tatu mtoto wake alianza tabia ya kulia usiku wa manane.
“Hiyo tabia ya kulia amekuwa nayo miaka yote, tulikwenda kwa waganga lakini wapi! Tukahamia makanisani kwa wachungaji kidogo mtoto alipata nafuu mwaka jana.
“Mwezi Novemba tarehe kumi na moja, mwaka jana (2013) yule mwanamke alikuja hapa nyumbani na kuniambia kuwa, mguu ule ni wangu.
“Alikaa chini mimi nikiwa nafua, akaanza kuniambia ‘mjukuu wangu samahani, nimeona unateseka sana na mwanao, nataka nikurudishie kwani mimi uchawi sasa basi.’
“Nilishtuka, nikamuuliza bibi unasema nini? Akajibu, ‘n imekuja kukwambia huyu si mtoto ni picha tu, mtoto wako ninaye mimi nyumbani kwangu na nina watoto wengi ila wa kwako ananisumbua, bora uje umchukue kesho asubuhi,” alisema mama Andrea.
“Siku iliyofuata nilikwenda kwake, sikumwona mtoto ila cha kushangaza aliniambia kuwa yeye anajua kuroga lakini hajui kutegua, ana mganga wake yupo Songea (Ruvuma), atampigia simu aje amtegue mtoto wangu arudi katika hali ya kawaida,” aliongeza mama Andrea.
Mama huyo alisema kuwa aliporudi nyumbani, aliwaambia wazazi wake kilichotokea na maneno yote waliyoongea na mwanamke huyo.
Wazazi wa mama Andrea walimuita mwanamke huyo akiwa na mumewe na mtoto wao mmoja, wakamuuliza kuhusu madai hayo, akaomba msamaha kwa kilichotokea.
Sakata hilo likaenda Serikali ya Mtaa Misigani ambapo mwanamke huyo alikiri mara ya kwanza na kusema kuwa amempigia simu mganga wa Songea atafika wakati wowote.
“Cha kushangaza alikaa kwa nusu saa na kusema amewapigia simu ndugu zake wamesema huyo mganga amefariki dunia. Kila mtu alimuuliza amepigaje simu mbona wamekaa naye na hajatoka nje? Akanyamza,” alisema mama Andrea.
Mama Andrea alisema serikali ya mtaa waliliona sakata hilo ni kubwa na kuamuru babu wa Andrea (jina lipo) kuchukua barua kuipeleka kwenye Kata ili kesi ihamie huko.
Mama huyo alimalizia kwa kusema kuwa anashindwa cha kuamua kwani kwa maelezo ya mwanamke huyo hajui akubali mtoto Andrea si wake au la! 
Kwa msaada wa global publisher

HOT!!! WEMA NA DIAMOND WAMERUDIANA?!!

HOT!!! WEMA NA DIAMOND WAMERUDIANA?!! WEMA SEPETU AMEPOST VIDEO HIZI MDA HUU MOJA YAKE MOJA YA DIAMOND AKIWA KIFUA WAZI


Video hizi amepost mwanadada wemasepetu katika akaunti yake ya instagram,..moja ikimonesha yeye mwenyewe amelala kitandani, na baadae inasikika sauti ya mwanaume kwa mbali akiongea uku wema akiitika kwa kumsikiliza,. bila shaka mwamaume uyo atakuwa ni Diamond platinumz
video nyingine ni hii ikimuonesha diamond pia amelala kitandani  kifua wazi na badae kukiss kamera iliyokuwa ikimchukua kitandani hapo,..video hii iliambatana naujumbe wa wema aliouandika mwenywe instagram akisema:-

Friday, January 10, 2014

YAYA TOURE ASHINDA TENA KWA MARAYA TATU TUZO YA MCHEZAJI BORA BARANI AFRIKA

YAYA TOURE ASHINDA TENA KWA MARAYA TATU TUZO YA MCHEZAJI BORA BARANI AFRIKA

Yaya Touré, kiungo wa Ivory Coastamechaguliwa kwa mara ya tatu kama mchezaji bora wa mwaka barani Afrika
Mchezaji huyo ameshinda baada ya kupigiwa kura na makocha wa timu za taifa za Afrika. Abedi Pele wa Ghana alishinda tuzo hiyo kwa mara tatu mfululizo kuanzia 1991–93 wakati mchezaji wa Cameroon Samuel Eto’o akishinda kuanzia 2003-05 na kushinda tena mwaka 2010

UMEWAHI KUJIULIZA KWANINI NYIMBO AU VIDEO ZA "DIAMOND" AZIPIGWI "CHANNEL TEN" AU "MAGIC FM" KWA MWAKA SASA, BASI LEO AMEWAOMBA MSAMAHA LIVE HEWANI .SOMA ZAIDI HAPA

UMEWAHI KUJIULIZA KWANINI NYIMBO AU VIDEO ZA "DIAMOND" AZIPIGWI "CHANNEL TEN" AU "MAGIC FM" KWA MWAKA SASA, BASI LEO AMEWAOMBA MSAMAHA LIVE HEWANI .SOMA ZAIDI HAPA

Diamond akiwa katika studio za Magic FM

Diamond-magic1
Kama umewahi kujiuliza kwanini ulikuwa husikii nyimbo za Diamond Platnumz kupitia kituo cha Magic FM cha Dar es salaam pamoja na kituo cha TV Channel Ten kwa kipindi kirefu, jibu ni kwamba msanii huyo ambaye nyota yake inazidi kung’ara kila kukicha aliwahi kukikosea kituo hicho, kwa lugha ya mtaani ‘alizingua’.
Kwa mujibu wa Salmamsangi.com, Jumatano ya wiki hii (Jan 8) kupitia kipindi cha Daladala Beats cha Magic FM, Diamond akiwa Live kwenye kipindi hicho aliomba msamaha na kusema kuwa alikuwa na tofauti na Radio hiyo kutokana na mambo ya kibinadamu.
Diamond ambaye wiki hii ameachia video na audio ya ‘Number 1 RMX’ aliyomshirikisha Davido wa Naija, alifika katika studio za Magic akiwa ameongozana na Meneja wake Babu Tale wa Tip Top Connection pamoja na Said Fella.
Baada ya kuomba msamaha hewani sasa nyimbo za Platnumz zimeanza kupata airtime kupitia vipindi mbalimbali vya Radio hiyo ambayo ilisitisha kupiga kazi zake kwa takribani mwaka mmoja na nusu toka tofauti hizo zilipojitokeza.